mafanikio aliyo nayo mtu, yana tokana na nguvu za kiroho alizo nazo mtu.
Kila mtu anao upande mmoja wa kiroho kati ya mbili, ambapo ndipo huenda kuchukua mafanikio yake.
Kuna nguvu aina mbili za kiroho, ambazo ili mtu afanikiwe katika maisha ya hapa duniani, ni lazima awe upande mmoja katka hizi mbili.
Nguvu zenyewe ni _MUNGU na SHETANI.
hizi nguvu zote zinatenda kazi, lakini hazipatani.
Hivyo mtu hawezi kufanikiwa Kama hayupo upande wowote mmoja wapo, na wala haiwezekani mtu kuwa pande zote mbili kwa wakati mmoja, ni lazima mtu awe upande mmoja.
Kila nguvu inayo nafasi ya kutenda kazi kwa mtu alie upande huo, na alie tayari.
Kila upande wa nguvu hizi kunayo masharti, japokua masharti ya upande mmoja hayafanani na ya upande mwingine, ni tofauti kabisa.
Upande wa MUNGU masharti yake ni machache tu! Na tena yanafanana kwa watu wote wamuaminio, Kama ifuatavyo_
Usitende dhambi, usiache ibada yaani umuabudu MUNGU, usiwe mvivu yaani ufanye kazi zako na za MUNGU kwa bidii, usiache maombi, usisahau kutoa sadaka.
upande huu wa MUNGU hauna kafara, Kwani tayari MUNGU mwenyewe aliisha mtoa mwanae YESU KRISTO kuwa kafara pale msarabani kwa ajiri ya wote wamuaminio, hivyo hakuna sadaka ya damu (kafara).
Upande wa MUNGU upo msamaha, kwamba pindi mtu akisahau na kukosea/kutenda dhambi, akiomba msamaha/akitubu, MUNGU humsamehe mtu huyo, na wala hamfirisi/hamuondolei mafanikio aliyokua amempatia mtu huyo.
Upande wa SHETANI masharti yake sasa ni mengi mno, na hayafanani, mtu huyu anaweza kupewa masharti ya tofauti na ya mtu mwingine.
Kwa mfano_ huyu anaweza kuambiwa asiwe anakula nyama aina yoyote, asiwe anaoga ijumanne na ijumaa, asiwe anasafiri ijumanne, hayo tu!
Lakini mtu mwingine akapewa masharti tofauti kama vile_ asiwe analala juu ya kitanda, asitembee na mwanamke nnje/tofauti na mkewe, asinywe pombe, nk, ili mradi tu masharti yao hayafanani, hivyo kwa SHETANI masharti/miiko hua hayafanani, huyu hupewa tofauti na yule.
Kwa SHETANI kafara ni lazima, japokua mara nyingi kafara hutolewa kama adhabu, au hutolewa kama sehem ya matumizi ya utendaji kazi.
Kwa mfano_ mtu anaweza kutoa kafara ya damu ili mashetani wanywe wapate nguvu ya kumfanyia kazi yake ya mafanikio, kwakua damu ni Miongoni mwa vyakula pendwa vya kishetani.
Au kafara anaweza kutoa Kama adhabu ya makosa aliyo fanya, hasa kukiuka masharti aliyopewa.
Na kafara hazifanani, yaani kwa shetani mambo ni tofauti tofauti, huyu anaweza kuambiwa atoe damu ya njiwa mweupe au mweusi au mwekundu, mwingine akaambiwa atoe damu ya Kuku, au damu ya mbuzi, au damu ya n'gombe, au damu ya binadamu, hizo zote ni aina ya kafara.
Thamani ya damu inazidiana, na utendaji wa kazi zake nao unatofautiana, kwakua mafanikio yatakayokua kwa mtu alie toa kafara ya Kuku hayatakua sawa na yule alietoa kafara ya binadamu.
Kwa SHETANI hakuna msamaha, mtu akikosea ni adhabu tu! Tena wakati mwingine hata kunyan'ganywa yale mafanikio aliyokua kapewa.
Hivyo basi! Hakuna mtu anaeweza kufanikiwa kama hayupo upande wowote katika hizi mbili, ni lazima mtu awe upande wa MUNGU au upande wa SHETANI.
Hata Kama mtu ana kipaji, elimu, juhudi, bila kuwa na nguvu mojawapo ya kiroho katka hizi mbili, hawezi kufanikiwa.
Mafanikio yatokayo kwa MUNGU hayana majuto, lakini mafanikio yatokayo kwa SHETANI yana majuto makubwa Sana.
Hivyo basi! Ni vema mtu kumngoja MUNGU hata utakapofika wakati wake wa kubarikiwa na kuingia kwenye mafanikio, kuliko kufanya haraka kuyakimbilia mafanikio ya SHETANI ambayo huleta majuto, na mwisho wake hua ni m'baya zaidi.
(Elisha Emmanuel rutale)
Ushuhuda
JibuFutaNilivunjika kabisa uhusiano wangu ulipoisha. Niliamini kweli nimepoteza upendo wa maisha yangu milele. Kisha nikampata Dk. Dawn, na kila kitu kilibadilika.
Kwa fadhili, hekima, na mwongozo wenye nguvu, alinirudishia upendo ambao nilifikiri umetoweka. Leo, tuna furaha zaidi kuliko hapo awali!
Dr. Dawn kweli aligeuza machozi yangu kuwa furaha.
Dk. Dawn Anaweza Kukusaidia Na:
✅ Maneno ya mapenzi
✅ Tahadhari za Ujauzito
✅ Kurejesha Ndoa/Mahusiano
✅ Dawa za mitishamba kwa VVU, Ugonjwa wa Figo, Magonjwa ya Moyo, Maambukizi na mengine mengi.
📧 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
📞 Simu/WhatsApp: +2349046229159
Usiteseke kimya kimya. Dk. Dawn anaweza kurudisha furaha katika maisha yako!