Jumatano, 4 Oktoba 2017

NAMNA MTU ANAVYOWEZA KUZUIA BARAKA ZAKE NA KUHARIBU MAHUSIANO YAKE NA MUNGU

haijalishi mtu ameokoka, na anamuamini yesu kwa viwango gani! Lakini anaweza kuharibu mahusiano yake na MUNGU, na kuzuia baraka za MUNGU zisimfikie.

SABABU YA (1)
utamkuta mtu anatumia muda mwingi kufuatilia habari za watu wengine, kuliko kufuatilia habari za yesu kristo.
Mtu wa namna hiyo hujitahidi kuchimbua na kutaka kujua sili za maisha ya watu wengine_  wanatokaje na wanaingiaje, wanakula nini, wanavaa nini, nk, lakini hua hayuko makini kuangalia habari zake kwamba kwanini hapigi hatua, na kwa nini bado hajafika katika viwango anavyotamani kuvifikia kimaendeleo.
Hivyo basi! Huuutumia muda mwingi kujishughulisha kwa mambo  ya wengine, kuliko mambo Ya MUNGU na mambo yake mwenyewe, kwa sababu hiyo huharibu mahusiano yake na MUNGU,  na kuzuia baraka zake kutoka kwa BWANA.

SABABU YA (2)
Mtu anaejenga chuki dhidi Ya alie fanikiwa.
Utamkuta mtu anajenga chuki dhidi ya mtu aliefanikiwa, na kuanza kumuwazia na kumsema vibaya, badara ya kukuaa nae karibu ili achunguze na ajifunze namna gani alifanikiwa mwenzie.
Kwa namna hiyo mtu huyo huharibu mahusiano yake na MUNGU, na kuzuia baraka zake kutoka kwa BWANA.

SABABU YA (3)
kuingilia mahusiano ya mtu alie barikiwa na MUNGU wake.
Namaanisha (mtu na mungu wake).
Mtu anaweza kuzuia baraka zake, na kuharibu mahusiano yake na MUNGU pale tu! Anapojihusisha kuyasema vibaya mahusiano ya m'barikiwa na MUNGU wake.
Kwakua ikumbukwe kua kila jambo lina wakati wake, namaanisha kua kila mtu anao wakati wake wa kufanikwa, na kila mtu anao wakati wake wa kupokea baraka zake kutoka kwa BWANA, hivyo basi! Hakuna mtu mwingine anaeweza kuzuia baraka za m'barikiwa wakati ukifika.
Ispokua hasara yaweza kumpata mtu yule ambae huzidi kujitaabisha kwa kuyasema vibaya mahusiano ya   m'barikiwa na MUNGU wake, kwa kupoteza mahusiano yake na MUNGU na kujizuilia baraka zake mwenyewe.

KITU CHA KUFANYA ILI KUMALIZA TATIZO NI_
(1)kuishi maisha matakatifu.
(2)kumpenda m'barikiwa.
(3)kukaa karibu na alie barikiwa, ili kujifunza mbinu, maarifa, namna yeye alivyo weza kupokea baraka kutoka kwa BWANA.

Kwakufanya hivyo kunaweza kumfanya mtu awe na mahusiano mazuri na MUNGU wake, na kumfanya mtu huyo aweze kupokea baraka zake kutoka kwa BWANA.
❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni