Watu wengi wamekua wakishindwa kufanya biashara, kwa kudharau kiwango kidogo cha pesa (mtaji) walichonacho.
Wengine wanadhani kua ni lazima uwe na kiasi kikubwa cha pesa (mtaji) ndipo ufanye biashara, jambo ambalo sio sahihi.
Upo uwezekano wa mtaji mdogo kuufanyia biashara hata ukakua na kuzidi sana.
Pesa ndogo (mtaji) aliyonayo mtu anaweza kuifanyia biashara kwa viwango vilevile, kutokana na mazingira, na uhitaji wa watu waliopo sehem husika.
Kwamfano_ maeneo ya nyumbani, zinaweza kufanyika biashara kama vile, kuuza mkaa, kuuza matunda, kuuza nyanya vitunguu mbogamboga, kuuza vitumbua maandazi, na vitu vingine vidogo vidogo ambavyo ni mhim kwenye jamii inayoishi maeneo hayo.
Na biashara kama hizo hazihitaji mtaji mkubwa, bali kiasi kidogo tu cha fedha kinatosha kufanya hivyo.
Kwa mfano_ maeneo ya sokoni, zinaweza kufanyika biashara kama vile, kuuza samaki, kuuza mboga mboga, kuuza miwa, kuuza matunda, kuuza mchele, nk, biashara ndogo ndogo tu kulingana na mtaji alio nao mhusika.
Mfano_ Maeneo ya stendi ya mabasi au stesheni, zinaweza kufanyika biashara za kutembeza kwa namna ya umachinga kama vile, kuuza matunda, kuuza maji kandoro au maji poa, kuuza soda biskuti pipi keki, kuuza karanga.
Kuuza pafym betr mikanda porch toch memory card soks.
Biashara kama hizo hazihitaji mtaji mkubwa, bali fedha kidogo tu inaweza kufanya hivyo.
Wakati mwingine kinacho wafanya watu wasifanye biashara kwa kiwango cha pesa kidogo walicho nacho, ni kuzinyanyapaa biashara.
Kwani mtu mwingine hataki aonekane anauza mkaa, anahisi kua atashushwa thamani.
Au hataki kuuza karanga au ndizi au machungwa tena kwa kutembeza kwenye jua anahisi kama atadhalilika.
Mtu mwinge hataki hata kufanya biashara za kimachinga kwa kujiona kua yeye ni bora kuliko wengine, kumbe haohao wafanya biashara ndogo ndogo hufanya biashara kwa faida kabisa, tena kuna watu wamejenga nyumba za maana kwa kazi hizo hizo ndogondogo, tena kuna watu wanasomesha watoto wao kwa kazi hizo hizo.
Lakini mtu mjinga hudharau afanyacho mwingine.
Ni vizuri kijiuliza mbona yule anafanya kazi ile? Na huyu anafanya kazi hii? Kwanini, na ni kipi wanapata humo kwenye kazi hizo?
Na ni vizuri kujiuliza, mbona yule ni mtu kama mimi, tena ni kijana mwanamke au mwanamme kama mimi, mbona anafanya kazi ile, je! Mimi ni bora kuliko yeye?
Mtu akijiuliza maswali ya namna hiyo bila shaka atafunguka, atatoka kwenye giza la ujinga na kujua nini cha kufanya, na hata akiwa na kiasi kidogo cha pesa ataanza kukifanyia biashara yoyote itakayo kuwa sawa na kiwango kile, bila kujali anatazamwa vipi na watu.
Kumbe kiasi kidogo cha pesa kinaweza kufanya biashara kwa kiwango kama kilivyo, na hatimae kuja kuwa mtaji mkubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni