Hiki kisa unaweza Kusema ni hadithi tu! Lakini sivyo, bali ni kisa cha Kweli. Soma kwa makini, na ujifunze kutokana na makosa aliyoyafanya binti/mwanamke Kama wewe.
Kijana alikua muuza magazeti ya kutembeza mkononi (machinga).
Kwakweli hali yake ya uchumi haikuwa nzuri, Kwani mshahara wake ulitokana na idadi ya mauzo ambayo angeuza kwa siku, kipato hicho ndicho kilimuwezesha kupata mahitaji yake ya kila siku, pia kulipia kodi ya pango/nyumba aliyokua akiishi. Hakika kijana huyu alikua na hali ngumu, kwani chumbani mwake kulikua kuna ndoo mbili ndogo, moja ya kuogea, na nyingine maji ya kunywa, na kikombe kimoja tu!
Kijana huyu alikua na kitanda kisichokua na godoro, hivyo alitandika mkeka kwenye chaga, na usingizi ulikua unapita, na maisha yalikua yanaendelea.
Siku moja kijana akiwa kwenye harakati zake za kuuza magazeti, alimuona binti akiwa amesimama, akamsogelea,,,,,
Kijana,,,,,,,,,, habari yako,
nzuri,,,,,,,,,,,,,,,, aliitikia binti.
Kijana,,,,,,,,,,,,,Mbona umesimama hapa kwa muda nini shida?
Aah! Kuna mtu namsubiria,,,,,,,,,,alijibu binti.
Kijana,,,,,,,,,,,,,,,,Okay, ninaweza kujua wapi unapatikana ili baada ya kazi nikutafute, tuzungumze machache?
Binti,,,,,,,,,,,,,,,nisikudanganye, sio rahisi kunipata nyumbani, kwani wazazi wangu ni wakali sana, rabda nitakuja huku tena kesho tutaonana tutaongea.
Kijana,,,,,,,,,,,,,,,Pouwa! Mida gani?
Mida kama hiihiii!nitakuja,,,,,,,,,,,,,,alijibu binti huku akielekea kwenda kukutana na mtu aliekua amemsubiria, ambae alionekana ni mama wa umri kama mama yake.
Waliondoka, na kijana aliendelea na kazi yake ya kukata mitaa, kutafuta wateja wa magazeti yake
Kesho ilifika, na binti kwa uaminifu kabisa alifika sehem ile mida ile ile waliyo patana, muda kidogo kijana nae akawasiri.
Mambo,,,,,,,,,,,,kijana alimsalimia binti.
Pouwa,,,,,,,,,,,binti aliitikia.
Da! Mimi nilidhani hautakuja, nilijua umenidanganya, maana watoto wa mjini wengi waongoo!!!,,,,,,,,,,,aliongea kijana yule, huku akimpa ishara ya kua waondoke maeneo yale.
Binti,,,,,,,,,,,,,,,,kwa nini nikudanganye, kwa faida gani, kama ningerkua siji ningekuambia tu kwamba sitokuja.
Walielekea sehem kulipokua kunauzwa vinywaji, wakachukua viti na kuanza mazungumzo yao. Kijana akamuelekeza binti anapoishi, akampa na ratiba ya mida gani huwa anakua amekwisha rudi nyumbani ili binti aweze kumtembelea. Binti alimsihi kijana yule kwamba endapo atakua akienda kwake asiwe anamchelewesha kurudi nyumbani, Kwani wazazi wake ni wakali mno.
Kijana alimuahidi kufanya sawa na binti alivyo sema.
Wakaanza Mahusiano ya kimapenzi, wakapendana vilivyo, wala binti hakuona hali duni ya uchumi wa mpenzi wake kua ni kitu, japokua binti kwao mambo yalikua safi, na baba yake binti alikua mfanyakazi mstaafu, hivyo kwao na binti hakukua na shida ndogo ndogo, lakini tayari alikua amekolea kwa kijana maskini, muuza magazeti, mwenye kitanda kisichokua hata na godoro.
Mapenzi yaliendelea, lakini waswahili wanasema _PENZI NI KIKOHOZI HALIFICHIKI.
Tayari wazazi wa binti wakagundua kua binti yao anamimba. Tayari wakamfukuza nyumbani, binti akakimbilia kwa mpenzi wake, maisha ya mme na mke.
Kijana hakuwa na sufuria ya kupikia wala bakuli wala sahani wala mwiko, ilibidi waanze kuishi kwa kula mgahawani, baada ya siku chache walipata vyombo vya kuanzia maisha vile vya mhim kwanza, maisha yakaanza kusonga mbele.
Kijana aliendelea na kazi yake ya kuuza magazeti.
Siku moja kijana anafika ofsini kwao, anakutana na msiba, nani?, bossi wake amepata ajali na kupoteza maisha.
Wakafanya msiba, hatimae msiba ukaisha.
Sasa ofisi haina msimamizi, bossi, hivyo ikabidi mwenye kuihitaji nafasi ile ajaze fom, Miongoni mwa wachache walio jaza fom, kijana yule baba harusi mpya akaibuka ushindi na kua bossi. Furaha ya ajabu aliyo fika nayo nyumbani kijana yule, na kumhadithia mkewe jinsi ambavyo MUNGU amewakumbuka na wao.
Sasa maisha yalianza kubadilika, kijana akanunua vitu vyote mhim vya ndani, tayar nyumba waliyokuwa wakikaa ikawa haina kiwango chao, wakatafuta nyumba nzuri ya gharama, yenye hadhi, yenye usalama wa kutosha, maisha yakawa burudaani!!!
Kutokana na namna ambavyo kijana allipenda kazi yake, na kuifanya kwa ufanisi, alimpata tena nafasi ya kuwa mkurugenzi wa gazeti ya FEMA mkoa, hivyo yeye ndie aliekua mpokeaji, msambazaji, na msimamizi wa gazeti la FEMA katka shule zote za secondary mkoa wote.
Basi posho ikaongezeka, kipato kikapanda, ofsi yake ghorofa ya pili juu! Mambo yakawa good.
Kijana akaona sasa anapesa, hivyo ni vema amuwezeshe na mkewe, ili nae awe na kitu/kazi ya kufanya.
Mwanamke akaitaji apelekwe veta ili ajifundishe ufundi, veta akapelekwa, akawa fundi mzuri Sana wa cherehani.
Kijana akaona si vema mkewe afanye kazi moja tu ya ufundi, akamfungulia duka la nguo spesho, nnje mbele ya duka lake mwanamke akaweka cherehani, akawa akishona, na kuuza duka.
Siku si nyingi mwanamke akasema yeye kazi ya dukani na kushona hawezi, bora akae nyumbani alee mwenyewe watoto wake, kwani tayari walikua wameisha pata watoto wawili ambao walitafuta yaya akawa akibakia nao nyumbani
Mwanamme akasema sawa mke wangu, wewe ndie mke wangu kipenzi, tulieanza wote maisha ya taabu, chochote utakacho nitakufanyia.
Mwanamke akasema nataka nikae nyumbani niwe nauza maji baridi (kandoro) na ice cream, hivyo ninunulie Friji na friza, kijana akasema kwa hilo ondoa Shaka mke wangu nitafanya.
Mwanamke akarudi nyumbani akaanza kuuza maji na ice cream, kule dukani wakaweka mfanya kazi/ msaidizi, ambae pia alikua fundi ili kuitumia cherehani.
Mwanamke kafanya ile kazi, mara kazi ile nayo ikawa ngumu, akamwambia mmewe, hii kazi imenishinda ninachoka Sana mgongo kwa ajiri ya kukaa muda mrefu kufunga maji na ice cream, naomba tu niiache.
Mwanamme akasema ondoa Shaka mke wangu, wewe ndio mke wangu, na mama watoto wangu, mimi sjashindwa kuwatunza, na kumbuka tuliko toka na tulipo kwa sasa, hebu tulia lea/hudumia watoto wetu wafrahi na mama yao.
Mwanamke akawa mama wa nyumbani.
lakini kumbuka kua ukiwa hauna kazi, shetani nae atakupa kazi ya kufanya.
Mwanamke yule akaanza tabia za uzinzi/umalaya, ikawa mme wake akiondoka kwenda kazini, na yeye anaanza ujinga wake wa uzinzi.
Mwanamme akalijua hilo, kwakua alikua anampenda, alivyokua akikumbuka walipotoka kwenye hali mbaya ya uchumi, hakupenda kuchukua maamuzi ya haraka, bali aliendelea kuvumilia, huku akizidi kufanya uchunguzi, na kutafuta ushahidi wa yale anayo fanya mkewe, ili pindi atakapo fanya maamuzi kusiwepo lawama.
Mwanamke aliendelea na tabia yake ya uzinzi, hadi ilipofikia kukosa heshima kwa mmumewe.
Vituko vikawa haviishi ndani, mwanamke anamuinukia mmewe kwa matusi na kashifa, mara ooh! Mmewe hajui mapenzi, kwamba wapo wanaume wanao jua mapenzi na wala sio mmewe, sms zinaingia holela, simu zinapigwa bila mpangilio kutoka kwa wapenzi wake, mbele ya mmewe.
Kwakweli Vituko vilizidi hadi mwanamme akashindwa kuvumilia.
Siku moja nilikwenda kwao, kwakua yule kijana alikua rafiki yangu Sana, siku hiyo nilifika Kama kawaida sehemu ikiwa kwa rafiki yako wa kweli, unakua hauna mashaka ya mazingira, nikafika nasukuma mlango wa sebuleni ili niingie, ile tu naingia nilikutana na kituko cha ajabu pale sebuleni alichokua akikifanya yule Shemeji yangu,,,,,,,,
Nini nilicho kiona dhidi ya mwanamke yule?
Usikose kuwa nami pale nitakapo kuletea mkasa huu kwa awamu ya pili.