Rafiki ndie mtu pekee wa karibu.
Rafiki ndie msiri wa rafiki yake.
Ndio maana ni vema kuwa makini Sana wakati wa kuchagua rafiki, kwakua rafiki anaweza kukusaidia, pia rafiki anaweza kukuangamiza.
Unaweza Kua umeoa lakini mkeo akawa mkeo tu, na asiwe na sifa ya kuwa rafiki yako.
Unaweza kua umeolewa lakini mmeo akabakia kuwa mmeo tu, na asiwe na sifa ya kuwa rafiki yako Unaweza kubadilika kitabia au ukawa mwema, au ukawa m'baya kutokana na rafiki ulie nae.
Sio kila mtu alie karibu nawe anastahili kuwa rafiki yako, kwakua rafiki ni nafasi kubwa, na ya pekee ambayo kabla haujampa mtu nafasi hiyo unapaswa kumchunguza Kama anastahili kupewa, kwakua ndoa nyingi zimevunjika Kwasababu ya rafiki. Biashara nyingi zimekata kwa sababu ya rafiki. Hata kuna watu wameuwawa na marafiki walio waamini kabisa.
RAFIKI WA KWELI lazima ujue viwango vyake vya upendo Kwako. Ujue viwango vyake vya hekima na busara. Ujue kua kwake yapo mambo mazuri ambayo unaweza kijifunza, asiwe mwenye mambo ambayo ukiiga yatakuangamiza.
KWA MFANO_ akina Dada, rafiki yako akiwa kahaba/changudoa ni lazima nawewe utakua hivyo, kwa sababu upo muunganiko wa ushirikiano kwenye ulimwengu wa roho ambao lazima utajidhihirisha katika mwili.
MFANO_ akina kaka, kama rafiki yako akiwa teja/mwizi/mlevi/mvivu/nk, lazima na wewe utakua na tabia Kama zile, kwakua Miongoni mwa mambo ambayo marafiki hufanana ni pamoja na kuwaza, kula, kustarehe, nk.
Jambo la kufanya kabla hauja fanya maamuzi ya Yule kuwa rafiki yako, ni lazima ujue kua Je! Kuna mambo mema mazuri ambayo anayo rafiki yangu mtarajiwa, ambayo nitajifunza kutoka kwake? Je! Ni mazuri Kweli?
Na Kama rafiki yako mtarajiwa Hana sifa njema basi achana nae, pia nafasi ya urafiki usimpatie, kwakua ni HELI UWE PEKE YAKO, KULIKO KUWA NA RAFIKI WA HASARA NA WA KUKUANGAMIZA. rafiki mnafiki.
Jumamosi, 22 Aprili 2017
Rafiki wa kweli ni yupi?
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni