Watu wengi wamekua wakiteswa/wakiteseka na mapenzi, wengine wamesusa na kuapa kua hawatapenda tena! Lakini si Kweli Kwamba kufanya hivyo ndio suruhu ya maumivu yaliyo wahi kuwapata.
Kwa sasa nataka niwatahadharishe vijana wa kiume, kuhusu tabia ambazo zinaweza kuwasaidia kujua kama mpenzi alie nae hamfai endapo atamuona ana tabia Miongoni mwa hizi zifuatazo.
1_umekaa na mpenzi wako mahali frani, tangu mlipo kutana mpaka mnaagana vidole vyake havitulii kwenye cm, yeye ni kupokea sms na kutuma sms, na ukimtazama kwa makini unaona yuko busy na cm kuliko kua busy na wewe, ujue huyo hampo nae kwenye mapenzi ya Kweli, huenda wewe ni wa ziada.
2_hakupigii cm mpaka umpigie wewe, hata ukimtumia Salio hua hakupigii cm, mpaka wewe umpigie, ujue huyo hampo nae kwenye mapenzi ya Kweli, huenda wewe ni ziada.
3_anataka matumizi Kwako ya juu kuliko anavyo kiona kipato chako, sku usipo mtimizia mahitaji yake ya kipesa, anakususa kwa siku kadhaaa.
4_Pindi anapokukosea haombi msamaha, hapendi kuwa chini yako.
5_hapendi ushauri wako, na wala hajawahi kukuomba ushauri hata siku moja.
6_anapenda kukosoa maisha ya wengine, anajiona yeye ni bora kuliko watu wengine.
7_hua ukimpeleka nyumbani unapoishi lazima akosoe jitihada za mandhari yako, na kukuvunja moyo kwa kile ulicho jitahidi kufanya kadri ya uwezo wako.
8_hapendi kukushirikisha mipango yake ya kiuchumi, wakati mwingine hataki ujue kabisa!
9_hapendi uwe unakwenda nyumbani kwake, kwao.
10_hauna uhuru na cm yake huenda hata passward ya cm yake hauijui.
KAMA UTAONA TABIA HIZI KWA MPENZI WAKO BASI CHUKUA HATUA, KWAKUA HIZO NI DALILI TOSHA ZA KUJUA KUA HUYO NI MPENZI WAKO WA KWELI, AU NI JAMBAZI NA TAPELI LA KIMAPENZI.
hii inawahusu akina kaka kuwafaham wapenzi wao.
Jumamosi, 22 Aprili 2017
Tabia zitakazo kufanya umfaham mpenzi asie kufaa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni