Jumatatu, 24 Aprili 2017

HASARA ZA KIMAPENZI :

mapenzi ni kitu cha kuvutia na cha kupendeza, pale tu ambapo wapendanao walifanya maamuzi sahihi na yasiyokua na majuto.
Lakini mapenzi yana maumivu makubwa yanayo ambatana na hasara za mipango ya kimaisha, pale tu wapendanao wanapo anza kutofautiana.
Kuna watu wengi ambao mipango yao mingi na mikubwa imeharibika kwa sababu ya hasara za kimapenzi.
Kuna watu wamefirisika walikua na biashara kubwa kubwa, kuna watu wamepoteza hata nafasi zao za kazi kwa sababu ya hasara za kimapenzi.
Upo uwezekano mkubwa hata wa mtu kuukosa ufalme wa MUNGU, kwa sababu tu amevurugwa na mpenzi wake.

Kuna Ndugu mmoja mkoa (nauhifadhi) yeye alikua mfanya biashara mkubwa tu, lakini walipo anza kutofautiana na mkewe, mambo yalianza kuharibika.
Ilibainika kua mwanamke alikua akichota pesa kwa Siri na hatimae kwenda kujenga nyumbani kwao.
kwakua Mali ile waliitafuta wote, ilikua ngumu kwa Jamaa kumtoa kwenye biashara mkewe. Hivyo basi ilikua ni mashambulizi, kila mmoja akawa akiuza anachukua chake, hatimae biashara ikafika ukingoni, na Mahusiano ya mapenzi yao yakaishia Hapo.

Kuna binti mmoja alijinyonga kwa sababu ya mapenzi. Binti huyo alikua na Mahusiano na kijana ambae hakua mkweli, Kwani tayari kijana Yule alikua anamwanamke alimuacha kijijini kwao.
Kijana Yule alikwenda mjini kutafuta maisha, ndipo alipo kutana na yule binti na kuanza Mahusiano kisha wakaanza kuishi kama mke na mme.
Maisha yalikua mazuri kiasi kwamba Yule kijana alikua anakwenda kuchukua biashara nnje ya nnchi, na nguvu kubwa ya mtaji ilikua ya Yule binti, Kwani binti Yule alikua mfanyakazi kwenye kiwanda cha vinywaji, kitengo kikubwa tu cha mshahara wa kutosha.
Mapenzi yao yalikua moto moto, kwakua kila mmoja wao alijitahidi kumuonyesha mwenzie mambo mapya ya kimapenzi kila siku.
Binti alimpeleka kijana nyumbani kwao, na hatimae wakaowana kabisaa! Lakini kijana Yule alikua amekwisha oa mwanamke kijijini kwao, tena kwa ndoa halali ya kanisani. Na tena mkewe huyo alikuwa na watoto wawili.
Baada ya taalifa kufika kijijini kwao na kijana kua kwa sasa mambo yake ya kifedha yako vizuri, ilibidi mkewe huyo wa kijijini aende kumtafuta mmewe, na hatimae alimpata, na mmewe ilibidi amkaribishe nyumbani kwani hakuona vyema kuwakataa watoto wake ambao ni damu yake mwenyewe.
Jambo hilo likawa jipya na geni machoni pa binti Yule ambae ni mkewe mdogo wa mjini kwakua hakulijua toka mwanzo, yeye alijua kua yuko peke yake.
Kutokana na jinsi alivyo kua akiheshimika pale mtaani, na kazini kwake, na jinsi alivyo mpokea Yule kijana toka kijijini, na jinsi walivyokua wakishirikiana, na mipango na ahadi nyingi walizokua wameweka mbele yao, Yule binti alikosa uvumilivu, hatimae akaamua kujinyonga.
Ninayo mifano/visa vingi tu vya kuonyesha athari zinazo weza kumpata mtu endapo tu hakuwa makini kwenye maamuzi ya kuchagua mpenzi anaefaa.
Lakini ukweli ni kwamba zipo athari kubwa za kimapenzi zinazo weza kumpata mtu asipokua makini mwanzo.
Hauwezi kuwa baba wa familia bora Kama utakosea kwenye maamuzi ya kuchagua.
Hauwezi kuwa mama wa familia bora, kama utakosea kwenye maamuzi kuchagua.
Hauwezi kuwa na familia yenye malezi bora, kama ulikosea kwenye maamuzi ya awali.
Jamii inayo kuzunguuka, majirani, rafiki zako, wafanyakazi wenzio, hawawezi kukuheshim Kama haukuwa makini kwenye maamuzi yako ya awali ya kuowa/kuolewa, kwakua ili nyumba yako iwe imara ni lazima uwe makini Sana kwenye ujenzi wa msingi, lakini endapo tu utaboronga kwenye ujenzi wa msingi, basi nyumba yako /jengo,  haitakua imara, haitadumu muda mrefu, ipo sku itakuangukia na kukuaibisha.

        Uwe makini Sana unapofikia wakati wa kufanya maamuzi ya kuchagua mke/mme, kwakua ukikosea Hapo, umekosa, furaha, Heshima, pesa, afya, ufalme wa MUNGU, nk.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni