Jumatano, 24 Mei 2017

JE! MTU ANAWEZA KUFANYA BIASHARA KWA MTAJI MDOGO?

Watu wengi wamekua wakishindwa kufanya biashara, kwa kudharau kiwango kidogo cha pesa (mtaji) walichonacho.
Wengine wanadhani kua ni lazima uwe na kiasi kikubwa cha pesa (mtaji) ndipo ufanye biashara, jambo ambalo sio sahihi.

Upo uwezekano wa mtaji mdogo kuufanyia biashara hata ukakua na kuzidi sana.
Pesa ndogo (mtaji) aliyonayo mtu anaweza kuifanyia biashara kwa viwango vilevile, kutokana na mazingira, na uhitaji wa watu waliopo sehem husika.
Kwamfano_ maeneo ya nyumbani, zinaweza kufanyika biashara kama vile, kuuza mkaa, kuuza matunda, kuuza nyanya vitunguu mbogamboga, kuuza vitumbua maandazi, na vitu vingine vidogo vidogo ambavyo ni mhim kwenye jamii inayoishi maeneo hayo.
Na biashara kama hizo hazihitaji mtaji mkubwa, bali kiasi kidogo tu cha fedha kinatosha kufanya hivyo.
Kwa mfano_ maeneo ya sokoni, zinaweza kufanyika biashara kama vile, kuuza samaki, kuuza mboga mboga, kuuza miwa, kuuza matunda, kuuza mchele, nk, biashara ndogo ndogo tu kulingana na mtaji alio nao mhusika.
Mfano_ Maeneo ya stendi ya mabasi au stesheni, zinaweza kufanyika biashara za kutembeza kwa namna ya umachinga kama vile, kuuza matunda, kuuza maji kandoro au maji poa, kuuza soda biskuti pipi keki, kuuza karanga.
Kuuza pafym betr mikanda porch toch memory card soks.
Biashara kama hizo hazihitaji mtaji mkubwa, bali fedha kidogo tu inaweza kufanya hivyo.

Wakati mwingine kinacho wafanya watu wasifanye biashara kwa kiwango cha pesa kidogo walicho nacho, ni kuzinyanyapaa biashara.
Kwani mtu mwingine hataki aonekane anauza mkaa, anahisi kua atashushwa thamani.
Au hataki kuuza karanga au ndizi au machungwa tena kwa kutembeza kwenye jua anahisi kama atadhalilika.
Mtu mwinge hataki hata kufanya biashara za kimachinga kwa kujiona kua yeye ni bora kuliko wengine, kumbe haohao wafanya biashara ndogo ndogo hufanya biashara kwa faida kabisa, tena kuna watu wamejenga nyumba za maana kwa kazi hizo hizo ndogondogo, tena kuna watu wanasomesha watoto wao kwa kazi hizo hizo.
Lakini mtu mjinga hudharau afanyacho mwingine.
Ni vizuri kijiuliza mbona yule anafanya kazi ile? Na huyu anafanya kazi hii? Kwanini, na ni kipi wanapata humo kwenye kazi hizo?
Na ni vizuri kujiuliza, mbona yule ni mtu kama mimi, tena ni kijana mwanamke au mwanamme kama mimi, mbona anafanya kazi ile, je! Mimi ni bora kuliko yeye?
Mtu akijiuliza maswali ya namna hiyo bila shaka atafunguka, atatoka kwenye giza la ujinga na kujua nini cha kufanya, na hata akiwa na kiasi kidogo cha pesa ataanza kukifanyia biashara yoyote itakayo kuwa sawa na kiwango kile, bila kujali anatazamwa vipi na watu.

Kumbe kiasi kidogo cha pesa kinaweza kufanya biashara kwa kiwango kama kilivyo, na hatimae kuja kuwa mtaji mkubwa.

MATESO YA LAANA.

Laana ni nguvu ya uharibifu itendayo kazi, ambayo humpata mtu kutoka sehem frani, laana humpata mtu kwa kusababishwa.
Laana humtoa mtu kwenye mafanikio yake, laana hua inaharibu kila kitu kizuri cha mtu, laana pia ndio chanzo cha mikosi.

kazi ya laana ni nini?
Kazi ya laana ni kuharibu kabisa maisha ya mtu na kumfanya duni.
Kama vile_ mtu anaweza kuwa na laana ya umaskini, kila kazi atakayo ifanya haitampa kipato cha kukidhi mahitaji yake, maana yake laana inakula kipato.
Pia mtu anaweza akawa na magonjwa ya laana, magonjwa ya namna hiyo husumbua sana kwani hayawi kama magonjwa ya kawaida.
Pia mtu anaweza kuwa na tabia za laana, mtu wa namna hiyo lazima awe msumbufu dhidi ya watu wa karibu nae.
Yapo mambo mengine mengi ambayo yanaweza kumpata mtu kwa sababu ya laana, kama vile ajali, vifungo, utoro, misiba, nk, ili mradi tu ni mambo yanayo mtesa mtu.

Chanzo cha laana ni nini?  Au laana hutoka wapi?
Zipo sehem tofauti tofauti ambazo husababisha laana kwa mtu.

Kwanza_ mtu anaweza kupata laana kutoka kwenye ukoo wao, kwa akina baba na mama au babu, au baba wa babu yake. Huenda wazee wale kuna maagano waliyo wekeana na mashetani, hivyo mashetani huendelea kufuatilia maagano ndani ya kizazi hicho.

Namna ya pili_ mtu anaweza kupata laana ya kutamkiwa au kufanyiwa na watu wa kawaida tu kama maadui.

Namna ya tatu_ mtu anaweza kupata laana kwa dhambi zake mwenyewe alizotenda.

Namna ya nne_ mtu anaweza kuwa na laana ya bahati mbaya, kama vile anatembea njiani anapita sehem ambayo watu walienda kujioshea hizo laana na mikosi kwa waganga wa kienyeji, hivyo akazikwaa hizo laana kwa bahati mbaya.

Namna ya tano_ mtu anaweza akawa na laana ya kisasi dhidi ya watu alio wakosea, alio watendea vibaya, wakaamua kulipiza kisasi.

Mtu mwenye laana huishi maisha yasiyo na mafanikio, maisha ya umaskini, magonjwa, vifungo, utoro, misiba, upweke, ajali, wakati mwingine hata kuchukiwa na watu.

Mtu anaweza akawa ameokoka, hana dhambi, na mbinguni atakwenda, lakini akawa bado kuna laana Imemng'ang'ania bila yeye kujua.
Ipo namna ya kujiondoa katika laana, na kuwa huru kabisa, ni maombi, lakini ni maombi ya namna tofauti ambayo yanahitaji maarifa.
Sio kila maombi yanaweza kumtoa mtu kwenye laana.

             Somo hili litaendelea.

Jumanne, 23 Mei 2017

SABABU ZINAZOWEZA KUMFANYA MTU AWE MASIKINI NA MUHITAJI

Wakati mwingine umaskini au uhitaji wa mtu, hutokana na matokeo ya makosa anayofanya mtu mwenyewe, mhusika.
Kwakua huenda kukawa na furusa nyingi za kujikomboa, mtu anaziona, lakini mtu mwenyewe akawa hataki kuzitendea kazi, japokua hali yake ni duni, na yenye uhitaji mkubwa mno.
Basi umaskini na uhitaji unaweza kumuandama mtu wa namna hiyo kwa sababu ya ujinga wake mwenyewe, na wala mtu huyo asije mlaumu MUNGU.

baadhi ya mambo yanayoweza kumfanya mtu aendelee kuwa maskini na muhitaji ni kama haya yafuatayo_......

1_kuchagua kazi.
Kuna mtu hujifanya kuchagua kazi za kufanya, hutamani kufanya kazi kubwa kubwa, au zile zinazo onekana kua zenye kuheshimisha mbele za wengine, ili aonekane kua yupo juu, au ni mtu wa maana, hunyanyapaa sana kazi ndogondogo na kuwaona wanaozifanya kama hawana maana, au hawana thamani, au ni wajinga. Mtu wa namna hiyo hutamani mambo makubwa kabra ya wakati wake, hivyo husubiri sana kufikia viwango hivyo, bila mafanikio, hupoteza muda mwingi kwa kukaa na kungoja, na matokeo yake huambulia umaskini na uhitaji wa kutosha.

2_kuudharau mtaji mdogo.
Mtu mwingine hudharau pesa kidogo aliyonayo kwamba haiwezi kufanya biashara yoyote, hivyo huitumia hovyo hovyo na kuimaliza, huku akisubiria kupata pesa nyingi ili afanye biashara kubwa kubwa, huendelea kusubiria kupata mtaji mkubwa bila mafanikio yoyote, hatimae hali yake huzidi kuwa mbaya, hivyo umaskini na uhitaji wa kutosha huzidi kumuandama.

3_mtazamo wa kuajiriwa.
Mtu mwingine ameelekeza fikra zake kwenye kuajiriwa, na hana mtazamo wa kujiajiri mwenyewe.
Hivyo basi! Mtu wa namna hiyo huwa haisumbuwi akili yake kufikiria namna gani aweze kujiajiri, husubiria sana kupata ajira kutoka kwa watu wenye vipato, wenye nafasi zao, hungojea sana kwa muda mrefu bila mafanikio, mwishowe hali yake mtu wa namna hii huzidi kuwa mbaya, hivyo umaskini na uhitaji huzidi kumtesa mtu huyo.

4_uvivu.
Mtu mwinge anayo bahati ya kupendwa na watu, wanampatia kazi, ajira, lakini mtu huyo ni mvivu, hataki kujituma, hataki kufanya kazi kwa viwango vya kumridhisha tajiri yake.
Wakati mwingine hasara zinatokea kazini kwake kwa sababu ya uvivu unaopelekea utendaji kazi wake kuwa m'baya, hivyo matajiri kughaili kumuajiri kutokana na uvivu wake.
Ni mvivu hata kwenye kazi zake mwenyewe, hataki kufanya kazi kwa muda na wakati sahihi.
Mtu wa namna hiyo bila shaka atakua maskini na muhitaji wa kutupa.

5_matumizi zaidi ya kipato.
Matumizi zaidi ya kipato, yanaweza kumfanya mtu azidi kuwa maskini na muhitaji kila siku.
Kwa mfano kijana ana shilingi elfu kumi, anataka kuvaa 👖 jeans ya elfu kumi na nane, hivyo atakua mtumwa wa nguo, mpaka deni la elfu nane atakapo lipa.
Kwa mfano kuna mtu anapenda maisha ya mashindano katika matumizi, dhidi ya mtu wa wakaribu, bila kujua kua yule anaefanya nae mashindano anamzidi kipato, pia bila kuangalia kua matumizi anayofanya yatamuathiri kwa kiasi gani.
Pia mtu huyo anapenda starehe za anasa hata zina athiri kipato.
Hivyo huishi maisha ya umaskini na uhitaji kila siku.

Mtu yeyote anaweza kujikomboa dhidi ya umaskini na uhitaji, endapo tu ataamua kujikomboa.
Watu wengi wamekua wakidhani kua ni mpango wa mungu kuwa vile walivyo, kumbe inaweza ikawa sivyo, kwakua sio mpango wa MUNGU watu wawe maskini, bali WATU WA MUNGU WANA ANGAMIA KWA KUKOSA MAALIFA.
Badhi ya watu hudhani kua baraka za MUNGU huja kama miujiza, kumbe sivyo, baraka za MUNGU zitawafikia watu endapo watawajibika, watafanya kazi. Maana imeandikwa kua MUNGU atabariki kazi za mikono ya hao watakao fanya kazi, tena kwa bidii,  na sio kwa ulegevu. Hivyo basi! Mtu yeyote asie fanya kazi, asitegemee kuziona baraka za MUNGU kwake.
Kwakua ahadi za MUNGU kumuinua mtu yeyote kiuchumi ni lazima zipitie kwenye KUFANYA KAZI.

haijalishi ni kazi ya namna gani, maadam iwe kazi halali, inatakiwa mtu anaetaka kubarikiwa aifanye, bila kujali kutazamwa na watu, ili mtu huyo abarikiwe, na atoke kwenye umaskini na uhitaji.

Jumatatu, 22 Mei 2017

TOFAUTI YA MALAIKA NA MAJINI

kuna watu wanadhani majini ni viumbe wema, hata wamejitahidi kutengeneza mazingira rafiki dhidi yao na majini, lakini ukweli ni kwamba majini ni viumbe waovu ambao wapo upande wa shetani, hivyo mtu yeyote akijishikamanisha na majini amekua upande wa shetani.

CHIMBUKO LA MAJINI NI NINI?
hapo mwanzo kabla shetani hajamuasi MUNGU, majini walikua malaika.
Majini ni wale malaika walio muasi MUNGU wakiwa na shetani.
Shetani alipo asi, alianza kupiga kampeni /kuwalaghai malaika, na alifanikisha kwa sehem, alipata theruthi moja, yaani 1/3 ya malaika walio msikiliza na kua upande wake.
Hivyo katika idadi ya malaika wote walio kuwepo, MUNGU alibakia na theruthi mbili yaani 2/3 hao ndio malaika waliobakia na MUNGU mbinguni, ambao hawakukubali kushawishiwa na shetani.

Baada ya shetani kuasi, ilibidi afukuzwe mbinguni, ambapo alipewa makazi kuzimu chini ya aridhi, ambapo ndipo anapoishi yeye na wale malaika walio mkubali, ambao wanaitwa majini.
Majini hao ni watumishi wa shetani, kama vile malaika walivyo watumishi wa MUNGU.
Hivyo basi! Majini hutekeleza  kufanya kazi sawasawa na maagizo ya mkuu wao shetani.
Na ikumbukwe kua hakuna jambo jema kutoka kwa shetani, na tena majini hawawezi kufanya tofauti na na maagizo ya mkuu wao shetani.
Hivyo basi! Majini ni waovu kama alivyo mkuu wao shetani.

Kuna watu hua wanadhani majini ni viumbe wema, la! Hapana! Majini sio viumbe wema. Majini hujifanya wanamsaidia mtu, kumbe lengo lao ni kumtoa mtu karibu na MUNGU, ili mtu huyo awe upande wa shetani.
Ikumbukwe kua kama shetani alivyotamani kumiliki mbinguni akashindwa, basi! Tamaa yake bado inaendelea, na sasa anatamani watu wote wawe mali yake, ili MUNGU akose watu kabisaa! Lakini hatoweza kufanya hivyo kwakua MUNGU awajua walio wake.

Majini ni roho, roho inaweza kuvaa umbo la namna yoyote, jini linaweza kujigeuza binadam mwanamme au mwanamke, likaolewa au likaoa.
Lakini hayo yote haliyafanyi kwa wema, bali ni mbinu za kujiweka karibu na mtu ili limpate kirahisi.
Lakini malaika hawapo namna hiyo kwakua wao hawana kuoa wala kuolewa, bali wao huishi maisha matakatifu kama aishivyo MUNGU wao.

Hivyo basi! Mtu yeyote anaedhani kua eti majini ni viumbe wema, mtu huyo anakosea, au hajui, lakini kujua hutokana na kufundishwa, hivyo somo hili litamfanya aliekua hajui tofauti ya majini na malaika ajue, endapo atasoma somo hili.

Malaika ni watumishi wa MUNGU.
Majini ni watumishi wa shetani.
Hizo ni falme mbili tofauti, hazipatani, wala hazichangamani.

MUNGU YUPO KWA MTU KULINGANA NA VIWANGO VYA MTU AMJUAVYO MUNGU.

MUNGU yupo Kwa mtu, au MUNGU hutenda kazi kwa mtu, kulingana na viwango ambavyo mtu amempa, amemuamini, au amjuavyo.
Bila shaka hakuna jambo lolote gumu la kumshinda MUNGU, kila jambo ni jepesi kwa MUNGU.
ila kuna baadhi ya watu wamempa MUNGU nafasi kidogo ya utendaji kazi, kwamba yapo mambo awezayo kufanya, na mengine hawezi kufanya, utaskia wakisema_ jisaidie na MUNGU akusaidie, hiyo inamaanisha kwamba MUNGU anaweza kusaidiwa, kitu ambacho si sahihi.
Uweza wa MUNGU ni mkuu sana, hakuna jambo lolote linaloweza kushindana na uweza wa MUNGU likashinda.
Kwa mfano:..... Kuna watu wanaamini kwamba kwa jina la yesu mapepo yanaondoka na mtu anakua mzima, lakini watu haohao wanashindwa kuamini kua kwa jina la yesu mgonjwa wa ukimwi anapona.
Kwa mfano:...... Kuna watu wanaamini kwamba MUNGU anabariki, lakini haohao wanakwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta dawa eti za kuwafanya wafanikiwe.
Kuna watu wanaingia makanisani kwa bidii Sana lakini bado hawajavijua viwango vya MUNGU kwenye utendaji kazi wake.
Hakika ni hasara kubwa kwa watu ambao wana muda mrefu, pia wana bidii kwenda kanisani na kutoa sadaka, lakini bado hawakui katika imani ya kufaham viwango vya utendaji kazi wa MUNGU, kweli kuna hasara kwa watu wa namna hiyo, kwakua wanaweza kuzikosa haki zao kutoka kwa BWANA kwakua tu viwango vyao havikui katika kumjua MUNGU.

MUNGU hutenda kazi kwa mtu kulingana na viwango mtu amjuavyo.
MUNGU hua anaonekana kwa mtu kulingana na viwango vya imani alivyo navyo mtu mwenyewe.

Mtu alie okoka, akikaa kanisani kwa muda mrefu bila mabadiliko, ya kutoka sehem kwenda sehem nyingine, yaani kutoka chini kwenda juu, basi mtu huyo ni mzembe, tena ni mvivu wa kuyafanyia kazi yale ambayo hua anafundishwa kanisani.
Wapo watu watakao okoka nyuma yake, wakiyatendea kazi yale wafundishwayo, MUNGU atajidhihirisha kwao kwa viwango vikubwa, kuliko hata yule walie mkuta akiwa kanisani kwa muda mrefu.
Inashangaza sana mtu yupo kanisani kwa muda mrefu, miaka kadhaa, lakini mtu huyo hata kumuombea mgonjwa hawezi, Hata yeye kujiombea au kuiombea familia yake hawezi.
Tena inaskitisha mtu yupo kanisani kwa muda mrefu, miaka kadhaa, lakini bado hali ya uchumi ya mtu huyo ni duni. Wengine wanakuja nyuma yake, wanajifunza maarifa ya kimungu, wanayaweka kwenye vitendo, tayari wana inuliwa.

Kwanini watu wengi hawafiki kule wanapotaka kufika?
              Ni kwasababu hawamruhusu MUNGU awafikishe, bali wanaona kana kwamba MUNGU pekee hawezi kuwafikisha, ispokua wamsaidie.
Hiyo inatokana na kutojua ukuu wa viwango vya MUNGU vya utendaji kazi vile ulivyo.

Kuna watu wana matatizo makubwa makubwa, lakini wameshindwa kumkabidhi MUNGU matatizo yao, badara yake wameendelea kutafuta suruhu sehem mbalimbali ambapo hata msaada umekosekana kwa sababu hawampi MUNGU nafasi kubwa anayostahili ili awatatulie shida zao. Wanadhani MUNGU hawezi.

MUNGU pekee anajitoshereza. Hahitaji kitu au mtu yeyote kumsaidia, japo watu wengi wanadhani kwamba lazima kujisaidia ili na MUNGU awasaidie.
Ikumbukwe kua, MUNGU yuko juu ya vyote, na kila kitu kipo kwa uweza wake, je! Kuna jambo la kumshinda yeye? Hakuna.

Basi!
        MUNGU YUPO KWA MTU, KWA VIWANGO VILE MTU AMJUAVYO.