Jumatano, 24 Mei 2017

MATESO YA LAANA.

Laana ni nguvu ya uharibifu itendayo kazi, ambayo humpata mtu kutoka sehem frani, laana humpata mtu kwa kusababishwa.
Laana humtoa mtu kwenye mafanikio yake, laana hua inaharibu kila kitu kizuri cha mtu, laana pia ndio chanzo cha mikosi.

kazi ya laana ni nini?
Kazi ya laana ni kuharibu kabisa maisha ya mtu na kumfanya duni.
Kama vile_ mtu anaweza kuwa na laana ya umaskini, kila kazi atakayo ifanya haitampa kipato cha kukidhi mahitaji yake, maana yake laana inakula kipato.
Pia mtu anaweza akawa na magonjwa ya laana, magonjwa ya namna hiyo husumbua sana kwani hayawi kama magonjwa ya kawaida.
Pia mtu anaweza kuwa na tabia za laana, mtu wa namna hiyo lazima awe msumbufu dhidi ya watu wa karibu nae.
Yapo mambo mengine mengi ambayo yanaweza kumpata mtu kwa sababu ya laana, kama vile ajali, vifungo, utoro, misiba, nk, ili mradi tu ni mambo yanayo mtesa mtu.

Chanzo cha laana ni nini?  Au laana hutoka wapi?
Zipo sehem tofauti tofauti ambazo husababisha laana kwa mtu.

Kwanza_ mtu anaweza kupata laana kutoka kwenye ukoo wao, kwa akina baba na mama au babu, au baba wa babu yake. Huenda wazee wale kuna maagano waliyo wekeana na mashetani, hivyo mashetani huendelea kufuatilia maagano ndani ya kizazi hicho.

Namna ya pili_ mtu anaweza kupata laana ya kutamkiwa au kufanyiwa na watu wa kawaida tu kama maadui.

Namna ya tatu_ mtu anaweza kupata laana kwa dhambi zake mwenyewe alizotenda.

Namna ya nne_ mtu anaweza kuwa na laana ya bahati mbaya, kama vile anatembea njiani anapita sehem ambayo watu walienda kujioshea hizo laana na mikosi kwa waganga wa kienyeji, hivyo akazikwaa hizo laana kwa bahati mbaya.

Namna ya tano_ mtu anaweza akawa na laana ya kisasi dhidi ya watu alio wakosea, alio watendea vibaya, wakaamua kulipiza kisasi.

Mtu mwenye laana huishi maisha yasiyo na mafanikio, maisha ya umaskini, magonjwa, vifungo, utoro, misiba, upweke, ajali, wakati mwingine hata kuchukiwa na watu.

Mtu anaweza akawa ameokoka, hana dhambi, na mbinguni atakwenda, lakini akawa bado kuna laana Imemng'ang'ania bila yeye kujua.
Ipo namna ya kujiondoa katika laana, na kuwa huru kabisa, ni maombi, lakini ni maombi ya namna tofauti ambayo yanahitaji maarifa.
Sio kila maombi yanaweza kumtoa mtu kwenye laana.

             Somo hili litaendelea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni