MUNGU yupo Kwa mtu, au MUNGU hutenda kazi kwa mtu, kulingana na viwango ambavyo mtu amempa, amemuamini, au amjuavyo.
Bila shaka hakuna jambo lolote gumu la kumshinda MUNGU, kila jambo ni jepesi kwa MUNGU.
ila kuna baadhi ya watu wamempa MUNGU nafasi kidogo ya utendaji kazi, kwamba yapo mambo awezayo kufanya, na mengine hawezi kufanya, utaskia wakisema_ jisaidie na MUNGU akusaidie, hiyo inamaanisha kwamba MUNGU anaweza kusaidiwa, kitu ambacho si sahihi.
Uweza wa MUNGU ni mkuu sana, hakuna jambo lolote linaloweza kushindana na uweza wa MUNGU likashinda.
Kwa mfano:..... Kuna watu wanaamini kwamba kwa jina la yesu mapepo yanaondoka na mtu anakua mzima, lakini watu haohao wanashindwa kuamini kua kwa jina la yesu mgonjwa wa ukimwi anapona.
Kwa mfano:...... Kuna watu wanaamini kwamba MUNGU anabariki, lakini haohao wanakwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta dawa eti za kuwafanya wafanikiwe.
Kuna watu wanaingia makanisani kwa bidii Sana lakini bado hawajavijua viwango vya MUNGU kwenye utendaji kazi wake.
Hakika ni hasara kubwa kwa watu ambao wana muda mrefu, pia wana bidii kwenda kanisani na kutoa sadaka, lakini bado hawakui katika imani ya kufaham viwango vya utendaji kazi wa MUNGU, kweli kuna hasara kwa watu wa namna hiyo, kwakua wanaweza kuzikosa haki zao kutoka kwa BWANA kwakua tu viwango vyao havikui katika kumjua MUNGU.
MUNGU hutenda kazi kwa mtu kulingana na viwango mtu amjuavyo.
MUNGU hua anaonekana kwa mtu kulingana na viwango vya imani alivyo navyo mtu mwenyewe.
Mtu alie okoka, akikaa kanisani kwa muda mrefu bila mabadiliko, ya kutoka sehem kwenda sehem nyingine, yaani kutoka chini kwenda juu, basi mtu huyo ni mzembe, tena ni mvivu wa kuyafanyia kazi yale ambayo hua anafundishwa kanisani.
Wapo watu watakao okoka nyuma yake, wakiyatendea kazi yale wafundishwayo, MUNGU atajidhihirisha kwao kwa viwango vikubwa, kuliko hata yule walie mkuta akiwa kanisani kwa muda mrefu.
Inashangaza sana mtu yupo kanisani kwa muda mrefu, miaka kadhaa, lakini mtu huyo hata kumuombea mgonjwa hawezi, Hata yeye kujiombea au kuiombea familia yake hawezi.
Tena inaskitisha mtu yupo kanisani kwa muda mrefu, miaka kadhaa, lakini bado hali ya uchumi ya mtu huyo ni duni. Wengine wanakuja nyuma yake, wanajifunza maarifa ya kimungu, wanayaweka kwenye vitendo, tayari wana inuliwa.
Kwanini watu wengi hawafiki kule wanapotaka kufika?
Ni kwasababu hawamruhusu MUNGU awafikishe, bali wanaona kana kwamba MUNGU pekee hawezi kuwafikisha, ispokua wamsaidie.
Hiyo inatokana na kutojua ukuu wa viwango vya MUNGU vya utendaji kazi vile ulivyo.
Kuna watu wana matatizo makubwa makubwa, lakini wameshindwa kumkabidhi MUNGU matatizo yao, badara yake wameendelea kutafuta suruhu sehem mbalimbali ambapo hata msaada umekosekana kwa sababu hawampi MUNGU nafasi kubwa anayostahili ili awatatulie shida zao. Wanadhani MUNGU hawezi.
MUNGU pekee anajitoshereza. Hahitaji kitu au mtu yeyote kumsaidia, japo watu wengi wanadhani kwamba lazima kujisaidia ili na MUNGU awasaidie.
Ikumbukwe kua, MUNGU yuko juu ya vyote, na kila kitu kipo kwa uweza wake, je! Kuna jambo la kumshinda yeye? Hakuna.
Basi!
MUNGU YUPO KWA MTU, KWA VIWANGO VILE MTU AMJUAVYO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni