kuna watu wanadhani majini ni viumbe wema, hata wamejitahidi kutengeneza mazingira rafiki dhidi yao na majini, lakini ukweli ni kwamba majini ni viumbe waovu ambao wapo upande wa shetani, hivyo mtu yeyote akijishikamanisha na majini amekua upande wa shetani.
CHIMBUKO LA MAJINI NI NINI?
hapo mwanzo kabla shetani hajamuasi MUNGU, majini walikua malaika.
Majini ni wale malaika walio muasi MUNGU wakiwa na shetani.
Shetani alipo asi, alianza kupiga kampeni /kuwalaghai malaika, na alifanikisha kwa sehem, alipata theruthi moja, yaani 1/3 ya malaika walio msikiliza na kua upande wake.
Hivyo katika idadi ya malaika wote walio kuwepo, MUNGU alibakia na theruthi mbili yaani 2/3 hao ndio malaika waliobakia na MUNGU mbinguni, ambao hawakukubali kushawishiwa na shetani.
Baada ya shetani kuasi, ilibidi afukuzwe mbinguni, ambapo alipewa makazi kuzimu chini ya aridhi, ambapo ndipo anapoishi yeye na wale malaika walio mkubali, ambao wanaitwa majini.
Majini hao ni watumishi wa shetani, kama vile malaika walivyo watumishi wa MUNGU.
Hivyo basi! Majini hutekeleza kufanya kazi sawasawa na maagizo ya mkuu wao shetani.
Na ikumbukwe kua hakuna jambo jema kutoka kwa shetani, na tena majini hawawezi kufanya tofauti na na maagizo ya mkuu wao shetani.
Hivyo basi! Majini ni waovu kama alivyo mkuu wao shetani.
Kuna watu hua wanadhani majini ni viumbe wema, la! Hapana! Majini sio viumbe wema. Majini hujifanya wanamsaidia mtu, kumbe lengo lao ni kumtoa mtu karibu na MUNGU, ili mtu huyo awe upande wa shetani.
Ikumbukwe kua kama shetani alivyotamani kumiliki mbinguni akashindwa, basi! Tamaa yake bado inaendelea, na sasa anatamani watu wote wawe mali yake, ili MUNGU akose watu kabisaa! Lakini hatoweza kufanya hivyo kwakua MUNGU awajua walio wake.
Majini ni roho, roho inaweza kuvaa umbo la namna yoyote, jini linaweza kujigeuza binadam mwanamme au mwanamke, likaolewa au likaoa.
Lakini hayo yote haliyafanyi kwa wema, bali ni mbinu za kujiweka karibu na mtu ili limpate kirahisi.
Lakini malaika hawapo namna hiyo kwakua wao hawana kuoa wala kuolewa, bali wao huishi maisha matakatifu kama aishivyo MUNGU wao.
Hivyo basi! Mtu yeyote anaedhani kua eti majini ni viumbe wema, mtu huyo anakosea, au hajui, lakini kujua hutokana na kufundishwa, hivyo somo hili litamfanya aliekua hajui tofauti ya majini na malaika ajue, endapo atasoma somo hili.
Malaika ni watumishi wa MUNGU.
Majini ni watumishi wa shetani.
Hizo ni falme mbili tofauti, hazipatani, wala hazichangamani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni